Jeshi la polisi wilayani Makete mkoani Njombe linamshikilia Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa wilayani hapa kwa makosa mawili ya utekaji nyara na ubakaji kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.
Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba amesema kuwa siku ya tarehe 5 mwezi huu walipokea taarifa kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.
Amesema kuwa mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri kuwa amebakwa na hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.
Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu, na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3 mwezi Januari mwaka huu majira ya saa saba mchana mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana.
Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.