Tuesday, January 7, 2014

AKATWA MAPANGA NA MUMEWE KWA KUPINGA MTOTO WAO HASIKEKETWE

MKAZI wa Kitongoji cha Songa Mbele wilayani Tarime mkoani Mara, Modester Mwita,33, amepigwa panga na mumewe kwa madai kuwa hataki mtoto wake wa kike wa umri wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) kwenda kukeketwa.
Modester Mwita.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita akiwa Hospitali ya Bomani mjini hapa, Modester alisema kuwa tukio hilo lilitokea  asubuhi saa mbili Desemba,13, mwaka jana baada ya kukataa mtoto wake huyo asikeketwe.
“Nilimwambia mume wangu Mwita Daudi kwamba haiwezekani mtoto wetu kwenda kukeketwa kwa kuwa mila hiyo imepitwa na wakati jambo ambalo lilimfanya kupatwa na hasira na kunikatakata kwa panga mguu,” alisema.
Modester aliongeza kuwa alikuwa ameenda mnadani Nyamwigura kupeleka biashara siku ya Desemba 12, aliporudi jioni nyumbani alikuta binti yake na mumewe hawapo ndipo mdogo wake akamwambia mwanaye alipelekwa kukeketwa.

‘’Mume wangu aliporudi nyumbani asubuhi nilimuuliza alikokuwa mwanangu hakunijibu, nilipomueleza kuwa sitaki akeketwe akaanza kunipiga na kunikimbiza kwa panga,” alisema mama huyo na kuongeza:

“Aliponikamata alinikatakata mguuni, wasamaria wema wakanileta hapa Hospitali ya Bomani, yeye ametoroka na sijui hali ya binti yangu huko aliko ikoje,” alisema.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakupenda jila lake liandikwe kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi la polisi mkoani humo, amethibitisha kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa mtuhumiwa anasakwa ili aweze kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.
Blogger Tricks

Monday, January 6, 2014

Binti wa miaka 15 atekwa kwa siku tatu na kubakwa huko Makete, Njombe


 Na Edwin Moshi,Makete
Jeshi la polisi wilayani Makete  mkoani Njombe linamshikilia  Fransis Pilla (36) mkazi wa kijiji cha Iwawa na kata ya Iwawa  wilayani hapa kwa makosa  mawili ya  utekaji nyara na  ubakaji  kwa binti mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.
Akiongea na vyombo vya habari wilayani hapa afisa upelelezi wa jeshi la polisi wilaya ya Makete Bw Gozbert Komba  amesema kuwa siku ya tarehe 5 mwezi huu walipokea taarifa  kutoka kwa msamaria mwema ambaye pia ni mwajiri wake bw. Erick Mbilinyi (34) ya      mtendewa kutekwa na kufungiwa ndani ya nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake maarufu kwa jina la pagale ambapo walifika katika jumba hilo  na kumkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.
Amesema kuwa  mara baada ya kumkuta mtendewa huyo akiwa ametekwa walimhoji na yeye kukiri  kuwa amebakwa na  hajaoga tangu afanyiwe ukatili huo na hivyo kurahisishia  kupatikana kwa vipimo kutoka kwa madaktari kuwa ni kweli binti huyo amebakwa na kuongeza kuwa walikuwa wana mahusiano ya kimapenzi.
Katika hatua nyingine mrakibu huyo amebainisha kuwa  mtendewa huyo alisema kuwa alitekwa nyara kwa siku tatu,   na hajala chakula kwa siku zote hizo ambapo alitekwa nyara tangu tarehe 3  mwezi Januari mwaka huu  majira ya saa saba mchana  mpaka tarehe 5 mwezi huu majira ya saa saba na nusu mchana. 
Amesema polisi wanatarajia kumfikisha mahakamani siku chache zijazo

KASHFA NZITO!!! MEJA JWTZ ADAIWA KUUA MADENTI 2 NA KUJERUHI 3 KWA RISASI...SOMA ZAIDI HAPA



Jeneza lenye mwili wa Ibrahim Mohamed.

MKESHA wa Mwaka Mpya (2014) ulikuwa ni kilio, huzuni na majonzi kwa wakazi wa Pugu Kwamustafa, Ilala jijini Dar es Salaam kufuatia Meja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Rashid Musa (43) kudaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi hadi kufa madenti wawili na wengine watatu kujeruhiwa wakati wakisherehekea mwaka.



Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo.

 Madenti waliouawa ni Ibrahim Mohamed (16), wa kidato cha tatu na Abubakar Hassan (14), wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Kinyamwezi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio, Meja Rashid wa Kikosi cha Jeshi Land Force Kibaha, alidaiwa kuwamiminia risasi vijana hao waliokuwa wakishangilia kuuona mwaka mpya wakati walipokuwa wakivuka barabara.


 


Ibrahim Mohamed enzi za uhai wake.

 SHUHUDA NZITO

Kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha,  mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi liliwatafuta mashuhuda wa tukio hilo na kuzungumza nao wanachokijua.


 “Kwa jina naitwa Rashid Juma  nina miaka kumi na tatu, nakumbuka siku hiyo tulikuwa watoto wa kike na wa kiume, wengi wenye umri kati ya miaka nane hadi kumi na saba, tulikuwa kama themanini hivi, ilipofika saa sita kamili usiku tuliingia mitaani kushangilia kwa kuuona mwaka mpya.

 “Si mara ya kwanza sisi watoto wa mtaa huu kusherehekea mwaka mpya, kila mara tunafanyaga hivyo na kurudi majumbani salama, lakini nashangaa safari hii kipindi hiki hili balaa limetoka wapi?




Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.

 “Ilipofika saa sita na dakika tano tukiwa tunaendelea kusherehekea huku tukivuka barabara, tulipishana na gari la mwanajeshi huyo, hatukumtukana wala, ghafla tulisikia mlio wa risasi, paa! Paa! Papapa!

“Kabla hatujakaa sawa tulimwona mwenzetu (Abubakar) yupo chini huku akilia kwa uchungu akihitaji msaada, kabla hatujakaa sawa tena risasi ziliendelea kusikika, wengine wakiwa wamedondoka chini.


 Mimi na wenzangu wengine tulikimbia, tulijua ni majambazi,” alisema shuhuda huyo, akaendelea:
“Baada ya kutawanyika, tuliliona gari likiondoka katika eneo la tukio, tukapiga kelele, ndipo wazazi wetu wakatoka nje na kuliona lile gari. Wengine walilitambua kwa vile yule mwanajeshi anaishi karibu na maeneo haya, amekuwa akipita na gari lake hilo mara kwa mara.




Jeneza lenye mwili wa Ibrahim kabla ya maziko.

 “Hata hivyo, yule mwanajeshi  hakusimama, nasikia alikwenda hadi kwake, tulirudi na kuwaangalia waliopigwa risasi ndipo tuligundua kuwa wenzetu wawili walikufa na wengine walijeruhiwa.

 MAJERUHI AZUNGUMZA

Naye mmoja wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Agustina Pius alipohojiwa na paparazi wetu alisema siku ya tukio alikuwa nje ya nyumba yake akiongea kwa simu na ndugu zake wa mikoani akiwapongeza kwa kuuona mwaka mpya.


 “Ghafla nikasikia  milio ya risasi barabarani huku watoto waliokuwa wakisherehekea wakipiga kelele za kusema tunakufa…tunakufa,” alisema majeruhi huyo.

Aliendelea kusema kwamba kufuatia hali hiyo, aliweka simu kwenye mfuko wa suruali na kuingia ndani, lakini ghafla alisikia kitu kimepiga simu yake na kulipuka.


 Aliitoa  mfukoni ikiwa inawaka moto na kuitupa chini, alipojikagua ndipo aligundua anatokwa na damu nyingi kwenye paja, alipoangalia chini aliona risasi.

“Niliwaambia watu wa jirani yangu ambapo walinikimbiza Hospitali ya Amana kwa matibabu,” alisema.


 BABA MZAZI WA MAREHEMU

Naye baba mzazi wa marehemu Abubakar, mzee Hassan alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema ni tukio la ajabu sana kwake kwani watoto hao kila mwaka katika kuukaribisha mwaka mpya hutoka nje kuushangilia, anashangaa kusikia wameuawa kwa risasi.


 KAMANDA MINANGI

Jumamosi iliyopita, paparazi wetu alimfuata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Afande Marietha Minangi Komba na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alikiri kulipokea, akasema:


 “Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba meja huyo alifyatua risasi hewani kwa kudhani kuwa wale  vijana walikuwa wahalifu, hivyo alikuwa akijihami.

 “Kwa sasa tunamshikilia (meja). Wakati wa kukamatwa kwake bastola yake ilikuwa na risasi kumi, tano zilitumika katika eneo la tukio. Jeshi langu linaendelea na uchunguzi na sheria itachukua mkondo wake,” alisema kamanda huyo.

WALIOJERUHIWA 

Waliojeruhiwa katika sakata hilo ni  Lugano Wanga (17), Kasim Abdul (16) na Agustina Pius (28) ambao walikimbizwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na kuruhusiwa.


-credit: GPL

SAKATA LA MADAWA!!!! JACK PATRICK MAZITO TENA....KESI KUSIKILIZWA 2016, MAASKOFU TUMBO JOTO...SOMA ZAIDI HAPA

HABARI mpya za supastaa modo wa Bongo aliyedaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Macau, China, Jacqueline Patrick ‘Jack’(pichani) zinazidi kumuumiza mrembo huyo.

Jacqueline Patrick ‘Jack’.
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za unga aina ya heroin tumboni zikiwa na thamani ya shilingi milioni 300.

TAARIFA MBICHI

Taarifa mbichi kabisa zinadai kwamba, Jack amepewa mwaka mmoja na nusu (siku 447) ajifunze lugha inayozungumzwa na watu wa Macau (Kireno) ambayo ndiyo itakayotumika mahakamani wakati kesi yake itakapoanza kuunguruma.

 

Dawa za kulevya alizokutwa nazo Jack Patrick.
Sheria ya kisiwa hicho inasema kuwa mshitakiwa yeyote atakayefikishwa kortini, kesi yake haitasikilizwa mpaka majaji wakubali kwamba anajua lugha hiyo na si kinyume na hapo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mwalimu maalum anayejua Lugha za Kiingereza na Kireno ndiye atakayemfundisha Jack mpaka atakapojua.

AKIJUA MAPEMA ITAMSAIDIA

Habari za ndani kutoka vyanzo vya uhakika nchini humo zinasema kwamba, kama Jack angekuwa anakijua Kireno angepandishwa kizimbani mara baada ya upelelezi kukamilika, Machi mwaka huu.

KIFUNGO CHA CHINI MIAKA 16

Habari nyingine mpya kutoka Macau zinasema kuwa, sheria za eneo hilo kuhusu makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya, mtuhumiwa akitiwa hatiani kifungo cha chini ni miaka 16 kulingana na mwenendo wa kesi.

SERIKALI YA TANZANIA YASUBIRI ORODHA…

Juzi,  paparazi wetu aliwasiliana kwa simu ya mkononi na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu nini kinaendelea kati ya serikali na utawala wa Macau kufuatia Mtanzania, Jack Patrick kunaswa na unga nchini humo.

Nzowa: “Aaah! Sisi tumetuma maswali yetu kule (Macau) kupitia Polisi wa Kimataifa (Interpol), tumetaka kujua kama huyo binti (Jack) amewataja vigogo waliomtuma ni majina gani wanayo.

“Ndiyo tunasubiri majibu yao ili tujue nini kinaendelea kule. Kama aliwataja watu tutaanza kuwafuatilia mara moja maana lazima kuna vigogo nyuma yake.”

KWA NINI MABOSI WA KUBEBA UNGA HUWA HAWATAJWI?

Kinachomshangaza Kamanda Nzowa ni usiri wa watu wanaodaiwa kukamatwa na unga kufunga vinywa vyao kuwataja vigogo waliowatuma.

Inadaiwa moja ya kiapo kikubwa kabla mtu hajaanza kuwa ‘punda’ (kubebeshwa madawa ya kulevya) ni kusema ‘piga, ua, galagaza’ katu hawezi kutaja wahusika wenye mzigo.

“Unajua kwa sababu gani? Wale wanaobeba wanaambiwa mkikamatwa msitutaje hata iweje ili tufanye mipango ya kuwatoa. Sasa mtu anaona nikitaja sintatoka, ndiyo anaamua kuendelea kuishi na siri yake halafu na wao wakubwa wao wanakuwa hawana habari nao,” alisema Nzowa.

KUMBE JACK ALIPEWA MAJI YA MOTO

Habari zaidi zinasema kuwa, siku ya tukio la kukamatwa, Jack alikataa kwamba hajabeba kete za unga tumboni, askari wa uwanjani wakampa maji ya moto ili anywe.

“Kwa mtu aliye na kete tumboni, hawezi kukubali kunywa maji ya moto kwani huyeyusha kete zilizomo ndani na kuweza kusababisha kifo chake.

“Jack alikataa kunywa maji ya moto, hilo likachangia askari kuamini ana kete tumboni, ndiyo maana walimpeleka chooni kuzitoa kitaalam,” kilisema chanzo.

RAY C AWASHANGAZA WENGI

Kufuatia sakata la Jack, hivi karibuni, staa wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliingiza kwenye mtandao wake wa kijamii akitoa maoni kwamba Jack apewe adhabu kali zaidi ya kifungo (pengine kunyongwa) hali iliyowashangaza wengi waliotembelea mtandao huo.

Baadhi ya watu waliozungumza na paparazi baada ya staa huyo kuingiza mawazo yake walimshutumu wakisema alitakiwa kutafakari upya.

“Yule dada (Ray C) hakutakiwa kumtakia mwenzake mabaya zaidi, kama yeye aliathirika na madawa na amepona anatakiwa kuwa balozi kwa wengine na si kuwahukumu wenzake,” alisema Joan Mushi, mkazi wa Sinza ‘E’ jijini Dar.

WAZIRI MEMBE VIPI?

Juzi, paparazi wetu alimtafuta Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamillius Membe ili azungumze lolote kuhusu sakata la Jack Patrick lakini hakupatikana badala  yake naibu wake, Mahadhi Maalim alisema taarifa za Jack kukamatwa amezisikia  kupitia vyombo vya habari na hana habari kiundani ila bosi wake anaweza kuwa na maelezo zaidi.

WOLPER, AUNT EZEKIEL, WEMA, WANAWINDWA KUWA ‘MAPUNDA’

Wakati Jack akiwa katika mazito hayo, habari ambazo zilifika kwenye dawati la paparazi wetu dakika za mwisho zinasema mastaa wa filamu za Bongo, Jacqueline Massawe Wolper, Aunt Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu wamekuwa wakitolewa udenda na vigogo wa unga.

Vigogo hao wamekuwa wakihaha kutafuta namna ya kuwaingiza mastaa hao kwenye ‘chaneli’ yao ili wawe mapunda wa kubeba kete za unga kupeleka ughaibuni wakiamini kuwa, mastaa hawakamatwi hovyo uwanja wa ndege, hususan wa Dar es Salaam.

-GPL

HUU NDIO UKWELI JUU YA KIFO CHA MSANII ZAY B ....BAADA YA KUZUSHIWA KIFO

Tumefatilia taarifa za kifo cha msanii Zay B toka taarifa hizi zianze kusamba asubuhi ya Tarehe 5/1/2014.

 


Taarifa hizi inasemekana zimetangazwa na kituo cha radio Hapa Tanzania kuwa msanii Zay B Amefariki na baada ya muda mfupi message na simu za pole zikamiminika kwa familia ya Zay B bila kujua kinacho endelea.

tumezungumza na mmoja ya Wanafamilia ya Zay na kupata ukweli kuwa yuko hai na salama kabisa. Hii ni post yake kwenye kurasa yake ya Facebook saa mbili zilizo pita


HUYU NDIYE KAJALA MASANJA...MFAHAMU HISTORIA YAKE NA FAMILIA YAKE


HII ni safu mpya ambayo itakuwa ikizungumzia juu ya maisha ya kweli ya mtu yeyote maarufu. Itatokana na mahojiano ya ana kwa ana!


Kwa kuanzia, tunaye nyota wa filamu za hapa nyumbani, Kajala Masanja, ambaye kabla ya kujiingiza kwenye sanaa hiyo aliwahi kuishi kinyumba na mmiliki wa studio ya Bongo Records, Paul Matheas, maarufu kama P.Funk na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Paula.

Katika safu hii, Kajala ambaye amewahi kukutwa na misukosuko lukuki ikiwemo kuhukumiwa kifungo jela, anaelezea mambo mengi kuhusiana na maisha yake ambayo hakuwahi kuyaelezea kokote kule au katika chombo chochote cha habari.
 

“Nilizaliwa mwaka 1983 katika familia ya mzee Masanja na walijaaliwa kuwa na watoto wawili tu, mimi na mdogo wangu, Dorice. Sisi tuna tofauti kubwa sana ya umri kati yetu kwa vile tulipishana sana kuzaliwa. Wakati nikizaliwa, wazazi wangu ambao wote ni askari polisi, walikuwa wakifanya kazi na kuishi kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
“Kutokana na kukaa muda mrefu utotoni nikiwa peke yangu, matokeo yake nilijikuta nikiishi kwa kudekezwa sana. Nilipofikisha umri wa miaka sita, nilipata shauku ya kuanza shule kwani nilikuwa nafurahi sana kuwaona watoto wenzangu wakipita pale wakienda na kurudi shuleni.

“Baada ya kuandikishwa Shule ya Msingi Mbuyuni, siku ya kwanza niliyotakiwa kwenda niliamka asubuhi na mapema na dada aliyekuwa akinilea alinivalisha nguo za shule na kunitaka sasa kusubiri chai kabla ya kunipeleka shuleni.
 

“Wakati dada akiipua chai ili animiminie kwenye kikombe, kwa bahati mbaya ilinimwagikia mapajani na kuniunguza sehemu kubwa ya mapaja yangu. Ikabidi wazazi wangu wafuatwe kituoni hasa kwa kuwa hakukuwa mbali na nyumbani, ambao walifika na kunipeleka hospitalini. Ndoto ya kusoma ikaishia hapohapo!
 

“Nilipofika hospitali, walinipa dawa na kila siku nilikuwa nikienda kuosha kidonda, hamu ya shule ikaniishia, nikawa mtu wa kulala tu, maana hata kutembea nilikuwa siwezi, kwani nilipohitaji kutembea nilibebwa na kufanyiwa kila kitu hadi nilipopata nafuu.
 

“Hali yangu iliendelea kuimarika hadi nilipopona kabisa na kuanza kwenda shuleni, ambako nilikutana na watoto wenzangu ambao tukajikuta tukijenga urafiki. Nilikuwa mpole mno, sikuwa mtu wa kuongea kabisa na mara nyingi watoto wenzangu wakorofi walipenda sana kunichokoza.
 

“Wakati huo nikisoma, mwalimu wangu wa darasa alikuwa Mama Salma Kikwete ambaye sasa ni first lady na nilikaa dawati moja na watoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan na Miraji na kwa kweli walikuwa ni marafiki zangu wakubwa sana.
 

“Nakumbuka nilipofika darasa la sita, kuna msichana mmoja alipanga kunipiga yeye na marafiki zake kwa madai kuwa mimi nimemchukulia mchumba wake, maana kipindi hicho ni wadogo na kutokana na upole wangu niliwaambia mimi sijafanya hivyo wakaniambia kesho yake lazima wanipige, maana enzi hizo tukitaka kupigana, lazima iwe Ijumaa.
 

“Siku hiyo ilipofika, mama alikuja kuniamsha asubuhi kwa ajili ya kwenda shuleni, nikajifanya nimebanwa na tumbo, siwezi kuamka wala kutembea, akanitafutia dawa na kunipa ninywe kisha akaniambia nilale. Nilishukuru sana kwani siku hiyo niliepuka kipigo.
 

“Ilipofika Jumatatu nikaendelea na mambo yangu kama kawaida wala hawakunisemesha tena, lakini nilikuwa muoga sana, nilijua wakati wowote wanaweza kunivizia na kunipiga, lakini haikutokea ingawa hata mimi rafiki zangu walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kujibu mashambulizi.
 

“Niliendelea kusoma shuleni hapo kwa amani mpaka nilipomaliza darasa la saba. Wakati huo nilikuwa na rafiki yangu mmoja wa kiume ambaye kila siku jioni alikuwa akipita nyumbani. Baba yangu akamshtukia, siku moja alichukua manati yake aliyokuwa akiitumia kuwapigia kunguru, alipopita akampiga nayo!
“Kufuatia kitendo hicho, rafiki yangu yule hakupita tena nyumbani na akatokea kunichukia sana kwa ajili ya kitendo alichofanyiwa, wakati wa kuanza sekondari ulipofika, nilipelekwa Songea katika shule ya masista kwa hofu kuwa nikisoma mjini nitaharibika kimaadili.

“Nilipoanza masomo shuleni hapo, nilikuwa mpweke sana maana sikuwahi kukaa mbali na wazazi wangu, halafu kulikuwa na baridi sana kitendo kilichosababisha nisiwe naoga kabisa na kujikuta nikipata ukurutu kwa uoga wa kuoga maji ya baridi.”  


PICHA ZA RAY C AKIMUONESHA MPENZI WAKE MPYA...ANGALIA PICHA 4 NA KAULI YAKE JUU YA HUYU MPENZIWE


http://distilleryimage9.ak.instagram.com/65053d0273b711e38b3d0e1d7b20dd35_8.jpghttp://distilleryimage4.ak.instagram.com/a7eba724745111e3983012127a964ccc_8.jpg


 

Mambomseto News Copyright © 2011 -- Template created by O Pregador -- Powered by Blogger

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter